kujadili juu ya maswala mbalimbali ya Wanawake ikiwemo maswala ya Kiuchumi, Kisiasa, Ukatili wa Kijinsia na Mipango mbalimbali iliyopo katika kuimarisha Jumuiya na kuendelea kumkomboa Mwanamke Kiuchumi, kisiasa na kijamii
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, amefika Ofisi za Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Makao Makuu Jijini Dodoma na kukutana na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Ndugu. Jokate Mwegelo.
Waziri Gwajima amefika Ofisini hapo kwa kuitikia wito wa Jumuiya hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake Taifa Mama Mary Chatanda (MCC) , wa kumtaka kufika ili kuzungumza na kujadili juu ya maswala mbalimbali ya Wanawake ikiwemo maswala ya Kiuchumi, Kisiasa, Ukatili wa Kijinsia na Mipango mbalimbali iliyopo katika kuimarisha Jumuiya na kuendelea kumkomboa Mwanamke Kiuchumi, kisiasa na kijamii ikiwa ni dhamira ya dhati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotokana na Chama Cha Mapinduzi.
Aidha, Wamejadili katika kuendelea kuhakikisha Wanawake wanainuliwa kiuchumi ikiwa ni dhamira thabiti ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan , katika kujenga na kuimarisha Jamii iliyo bora na rafiki kwa Watoto na Wanawake wote Nchini.