Onesheni utaalamu wenu, fanyeni kazi kwa vitendo ya kuwahudumia wananchi, badilikeni, fanyeni kazi kwa weledi na tambulikeni kwenye jamii kwa kuwa mfano bora kwa utendaji kazi wenu.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amekutana na kuzungumza na watumishi wa Wizara hiyo pamoja na watumishi wa Idara ya Ardhi kutoka jiji la Dodoma ambapo amewataka kuwahudumia wananchi kutatua migogoro ya ardhi katika maeneo yao.
Naibu Waziri Pinda amesema hayo Desemba 13, 2023 jijini Dodoma katika kikao cha kuhitimisha huduma za Kliniki ya Ardhi kilichofanyika katika Ofisi za Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Dodoma kuanzia Novemba 4 hadi Desemba 12, 2023.
“Onesheni utaalamu wenu, fanyeni kazi kwa vitendo ya kuwahudumia wananchi, badilikeni, fanyeni kazi kwa weledi na tambulikeni kwenye jamii kwa kuwa mfano bora kwa utendaji kazi wenu” amesema Naibu Waziri Pinda.