
Polisi nchini Somalia wamewakamata wafuasi wanne wa TikTok kwa madai ya kumtusi Rais Hassan Sheikh Mohamud kwenye video ya densi.
Katika chapisho hilo vijana kadhaa wanaonekana wakicheza wimbo mpya wa kampeni uliotumika awali wakati wa kuwania urais mwaka wa 2022, lakini maneno hayo yakiwa yamebadilishwa na kujumuisha lugha ya
Katika taarifa, polisi walisema washukiwa hao wako kizuizini na watafunguliwa mashtaka rasmi. Hawajazungumza lolote tangu kukamatwa kwao.
Washawishi kadhaa wa mitandao ya kijamii wamekamatwa na kufungwa jela hapo awali kwa kueneza matusi yanayotokana na koo, uchochezi au maudhui "ya uasherati" kwenye majukwaa kama vile TikTok - lakini hii ni kesi ya kwanza inayohusisha mwanasiasa mkuu.
Share: