Madereva hao wanasema barabara ya Arusha - Namanga imekuwa na vizuizi vingi barabarani
Wasafirishaji wa abiria na mizigo wanaofanya safari zao za kila siku kati ya Arusha na Namanga wilayani Longido, wamemuomba Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha kushughulikia changamoto mbalimbali wanazokutana nazo kwenye usafirishaji wa abiria na mizigo yao.
Madereva hao wanasema barabara ya Arusha - Namanga imekuwa na vizuizi vingi barabarani suala ambalo limekuwa likisababisha uzalishaji na ongezeko la rushwa na usumbufu kwenye shughuli zao.
Wakazi wengine wa Arusha pia wamezungumzia masuala ya usalama na changamoto ya Arusha kukosa kituo kikubwa cha Mabasi suala linaloshusha hadhi ya jiji hilo la Kitalii.
Wakazi hao pia wamemuomba Mkuu wa Mkoa Mh. Paul Makonda kuhamasisha wasaidizi wake kuwa na utamaduni wa kusikiliza kero za wananchi, wakimtaja kwa mfano Mkuu wa wilaya ya Longido Mh. Marco Ng'umbi kutokuwa msaada kwenye tabu zao.