Wapinzani wa sudan waanza mazungumzo ya kusitisha mapigano

Mazungumzo yaliyo rejewa baina ya wawakilishi wa jeshi linalo ongozwa na Abdel-Fattah Burhan, na kikosi cha dharura kinavyoongozwa na kamanda Hamdam Daglo, yanaendelea katika mji wa mwambao wa Saudia, Jeddah.

Katika taarifa, wizara ya mambo ya nje ya Saudi Arabia, inatarajia mazungumzo yatapelekea kufikia makubaliano ya kusimamisha mapigano, na pia upatanishi wa ya kisiasa yatakayo rejesha usalama, uthabiti, na ustawi kwa watu wa Sudan.

Mapigano ya Sudan yamesababisha watu milioni 4.5 kukimbia makazi yao kwenda ndani sehemu nyingine za Sundan, na zaidi ya watu milioni 1.2 kuwa wakimbizi katika mataifa jirani kwa mujibu wa shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa.

Share: