Wananchi morogoro wamuombea dua waziri silaa

Wananchi mkoani Morogoro wamefurahishwa na utendaji kazi wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa wa kutembelea maeneo yenye Changamoto za Ardhi kusikiliza na kutatua kero zao.

Waziri Silaa akiendelea na ziara yake mkoani humo mapema leo amefika katika kiwanja namba 33 Kitalu J chenye changamoto ya umiliki kati ya Shirika la Nyumba la Taifa NHC na kituo cha afya cha Ahmadiya health Centre kuhusu umiliki wa nyumba katika kiwanja hicho.

Kadhalika na pongezi hizo mmoja wa wamiliki hao anayefahamika kwa jina la Ayub amesema kuwa kwa zaidi ya miaka 30 hakuwahi kuona kiongozi amefika eneo hilo zaidi ya Waziri Silaa.

Ikumbukwe Kuwa Mwaka 1971 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitaifisha eneo la kiwanja hicho na kuliweka chini ya usimamizi wa shirika la nyumba la Taifa NHC.

Share: