Wanamgambo kongo washambulia na kuuwa watu 26

Washambuliaji wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wenye misimamo mikali ya dini ya Uislamu wamewaua watu 26 kwa kutumia panga usiku wa kuamkia Jumanne jana katika mji wa Oicha, mashariki mwa jahuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Jeshi la Kongo pamoja na meya wa mji huo wamethibitisha hayo na kulituhumu kundi la ADF kuhusika na shambulizi hilo.

Msemaji wa jeshi eneo hilo Antony Mwalushayi amesema shambulizi hilo dhidi ya raia, linaaminika kuwa ulipizaji kisasi dhidi ya mashambulizi ya hivi karibuni ya jeshi.

Share: