
Trump Rais wa Marekani, amesema atapeleka wanajeshi huko Washington DC, kama sehemu ya juhudi za serikali kukabiliana na uhalifu katika mji mkuu wa taifa hilo na watu wasio na makazi.
Trump amesema serikali ya shirikisho itachukua udhibiti wa Idara ya Polisi ya Washington DC,"Tutarudisha udhibiti wa mji wetu," Trump alisema Agosti 11 wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Trump amedai jiji hilo "limechukuliwa na magenge yenye kufanya vurugu na wahalifu wenye kumwaga damu.”
Lakini Meya wa DC, Muriel Bowser amekanusha madai hayo, kwani taarifa zinaonyesha uhalifu katika jiji hilo uko chini zaidi katika kipindi cha miaka 30.
Kwa upande mwingine, Waziri wa ulinzi wa Marekani, Pete Hegseth amesema “wanajeshi wataanza kumiminika katika mitaa ya Washington kuanzia wiki ijayo.”
Tangu Trump kuingia madarakani, wanajeshi wametumika huko Los Angeles kuzima maandamano ya kupinga maafisa wanaokamata wahamiaji.
Mara ya mwisho kwa wanajesh kutumwa Washington DC ni wakati wa uvamizi wa Januari 6, 2021, pale wafuasi wa Trump walipovamia majengo ya Bunge la Marekani.