Wakili amesema Jay Z na P Diddy hawana mahusiano mengine nje ya kazi

Katikati ya kesi inayoendelea ya madai ya ubakaji dhidi ya Jay-Z na Sean "Diddy" Combs, wakili wa Jay-Z, Alex Spiro, ametoa ufafanuzi kuhusu uhusiano kati ya wasanii hao wawili.

“Bw. Carter hana uhusiano wowote na kesi ya Bw. Combs au Bw. Combs mwenyewe,” alisema Spiro. “Walijuana kikazi kwa miaka kadhaa. Kama ilivyo kwenye taaluma nyingine, watu wanajuana. Wanapokutana kwenye tuzo za muziki, wanasaidiana. Wanaenda kwenye mechi za NBA All-Star, wanasaidiana. Hivyo ndivyo taaluma zinavyofanya kazi.”

Spiro alikanusha madai ya uhusiano wa karibu zaidi kati ya wawili hao, akiyaita hadithi za kubuni, na kusisitiza kuwa Jay-Z hana uhusiano wowote na mashtaka au madai yanayomkabili Diddy. “Hana uhusiano wowote na kesi hiyo na hakuna kingine cha kusema,” alihitimisha Spiro.

Wote wawili wanakabiliwa na madai yanayohusiana na tukio linalodaiwa kutokea mwaka 2000, ingawa Jay-Z amekanusha madai hayo vikali, akiyaita yasiyo na msingi na yanayochochewa na tamaa ya fedha na umaarufu. Kesi inaendelea huku pande zote zikiwasilisha hoja zao.

Share: