Wafungwa 2244 wasamehewa

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu December 09,2023 ametoa msamaha kwa Wafungwa 2,244 ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara.

Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni ambapo amesema kati ya Wafungwa hao waliopewa msamaha, Wafungwa 263 wataachiliwa huru December 09,2023, Wafungwa wawili waliohukumiwa adhabu ya kifo wamebadilishiwa adhabu ya kifo na kuwa kifungo cha maisha na Wafungwa 1,979 wamepunguziwa sehemu ya adhabu zao ambazo wataendelea kuzitumikia gerezani. 

“Ni matumaini ya Serikali kwamba wafungwa walioachiliwa huru leo tarehe 09/12/2023 watarejea tena katika jamii kushirikiana na wananchi wenzao katika ujenzi wa Taifa letu na kwamba watajiepusha kutenda makosa ili wasirejee tena gerezani”

Share: