
Rais wa Marekani, Donald Trump, amefanya mabadiliko makubwa katika Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) kwa kupunguza idadi ya wafanyakazi kutoka 10,000 hadi chini ya 300. Hatua hii inakuja baada ya USAID kutangaza kurejesha wafanyakazi wake waliokuwa nje ya Marekani, na kuwaweka wengine likizo.
Rais wa Marekani, Donald Trump, amefanya mabadiliko makubwa katika Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) kwa kupunguza idadi ya wafanyakazi kutoka 10,000 hadi chini ya 300. Hatua hii inakuja baada ya USAID kutangaza kurejesha wafanyakazi wake waliokuwa nje ya Marekani, na kuwaweka wengine likizo.
Kwa mujibu wa ripoti za New York Times na Reuters, #USAID sasa litabaki na wafanyakazi 294 duniani kote, wakiwemo 12 katika idara ya Afrika na wanane katika idara ya Asia. Aidha, serikaliya Trump imesitisha zaidi ya mikataba na tuzo 800 zilizokuwa zinasimamiwa na shirika hilo.
USAID, lililoanzishwa mwaka 1961 na Rais John F. Kennedy, ndilo shirika kuu la serikali ya Marekani linalosimamia misaada ya kimataifa na lilikuwa na bajeti ya dola bilioni 43.4 mwaka 2023. Sehemu kubwa ya fedha hizi zilitumika kusaidia utawala wa mataifa ya kigeni (dola bilioni 16.8 ), misaada ya kibinadamu (dola bilioni 10.5), afya (dola bilioni 7), na miradi ya kilimo, elimu, na miundombinu (dola bilioni 3.1).
Trump pia ameagiza kusitishwa kwa misaada yote ya maendeleo kwa siku 90, akidai kuwa USAID limekuwa likitumia vibaya fedha za walipa kodi. #ElonMusk, kupitia Idara ya Ufanisi wa Serikali (#DOGE), ameunga mkono hatua hiyo na kusema shirika hilo haliwezi kurekebishwa.
Wakati huo huo, Wizara ya Mambo ya Nje imechukua usimamizi wa muda wa USAID, huku Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio akiteuliwa kuwa mkurugenzi wa muda wa shirika hilo. Serikali ya Trump inatarajia kuliunganisha shirika hilo na Wizara ya Mambo ya Nje kwa lengo la kupunguza matumizi ya serikali.
Hatua hii pia imeathiri Mamlaka ya Ulinzi wa Mazingira (EPA), ambayo imetangaza kuwaweka wafanyakazi 168 kwenye likizo ya kiutawala ili kutii maagizo ya Trump kuhusu sera za utofauti, usawa, na ujumuishi. Serikali inaendelea na tathmini ya muundo wake ili kuhakikisha inatekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi.