Wafanyabiashara wa soko la kwa mrombo na murieti jijini arusha wamemshukuru rais samia suluhu kwa kuwatengenezea mazingira mazuri ya kufanya biashara zao

Wafanyabiashara hao pia wameahidi kumuunga mkono Mheshimiwa Rais na Mbunge wa Arusha Mjini Mheshimiwa Mrisho Gambo

Wafanyabiashara wa soko la Kwa Mrombo na Murieti Jijini Arusha wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa Arusha Mjini Mh. Mrisho Gambo, kwa kuendelea kupigania maslahi yao na kuwatengenezea mazingira mazuri ya kufanya biashara zao.

Wakizungumza na wanahabari wafanyabiashara hao wanaishukuru serikali kwa kurejesha mikopo ya asilimia 10 za Halmashauri na kusema kuwa mikopo hiyo imewaepusha na mikopo ya mtaani maarufu kama 'kausha damu' ambayo ilikuwa na riba kubwa kutokana na kutokuwa rasmi serikalini na hivyo kuathiri mitaji yao ya biashara.


Aidha wafanyabiashara hao pia wameishukuru serikali kwa miradi ya ujenzi na ukarabati wa masoko ya Jijini Arusha na hivyo kusaidia biashara zao kupata wateja zaidi na kuwaingizia kipato tofauti na ilivyokuwa awali.

Wafanyabiashara hao pia wameahidi kumuunga mkono Mheshimiwa Rais na Mbunge wa Arusha Mjini Mheshimiwa Mrisho Gambo kwa kuwapigia kura katika uchaguzi ujao wa mwaka 2025 kama sehemu ya shukrani kwa uaminifu wao katika utekelezaji wa ahadi walizoziahidi wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Share: