Waandishi wa habari 17 waliuawa wakiripoti kuhusu vita vya israel na hamas

Waandishi wa habari 17 wameuawa wakifuatilia vita vilivyoanza kati ya Israel na Hamas vilivyozuka tarehe 7 Oktoba, kulingana na shirika lisilo la kiserikali la Reporters Without Borders (RWB).

13 kati yao waliuawa katika Ukanda wa Gaza, RWB inasema

Lakini ikiwa utajumuisha waandishi wa habari waliouawa katika "mazingira ambayo hayajathibitishwa kuwa yanahusiana na majukumu yao", jumla ya wanahabari 63 wameuawa katika vita hivyo.

Data ilikuwa sahihi kufikia tarehe 1 Desemba.

Share: