Vita vya israel na gaza vitaendelea kwa miezi kadhaa, mkuu wa idf aonya

Vita vya Israel na wapiganaji wa Hamas huko Gaza vitaendelea kwa "miezi mingi zaidi", mkuu wa jeshi la Israel amesema. "Hakuna suluhu za kichawi," Herzi Halevi aliwaambia waandishi wa habari.

Siku ya Jumatatu Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu alionya kwamba operesheni "haijakaribia kuisha". Israel inasema ilipiga zaidi ya maeneo 100 siku ya Jumanne.

Inaripotiwa kuendeleza operesheni za ardhini hadi katikati mwa Gaza. Wizara ya afya ya Gaza inayoendeshwa na Hamas imesema Wapalestina 20,915 wameuawa katika zaidi ya wiki 11 za mapigano.

Vita vilianza tarehe 7 Oktoba baada ya Hamas kuongoza wimbi la mashambulizi mabaya kwa jamii ndani ya Israel. Takribani watu milioni 1.9 wamekimbia makazi yao kutokana na mashambulizi ya Israel tangu wakati huo, Umoja wa Mataifa unasema.

Juliette Touma, msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina (Unwra) aliiambia BBC: "Tunaona ripoti za kutisha sana za njaa katika baadhi ya maeneo, na wakati vita vinaendelea, uhamisho unaendelea na makazi ya Umoja wa Mataifa yamejaa na kuzidiwa. ."

Share: