Viongozi wa sekta ya afya simamieni ubora wa huduma za afya nchini

Naibu Waziri wa Afya Dk. Godwin Mollel, amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha wanasimamia ubora wa huduma katika Hospitali na Vituo vya kutolea Huduma za afya na kuhakikisha wanawajengea uwezo watumishi ili kuepuka changamoto na uzembe unaofanywa na baadhi ya wataalamu wa afya nchini. 

Dkt. Mollel ametoa agizo hilo leo Jijini Dar Es Salaam wakati akizungumza na watumishii wa afya katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke.

Dk. Mollel amesema yanapotokea matatizo katika vituo vya afya alafu Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya hawana taarifa au hawajachukua hatua hadi viongozi wa taifa wanafika watu hao wanatakiwa wajitafakari.

Amesema yanapotokea matatizo katika sekta ya afya pamoja na daktari aliyefanya uzembe watu wengine watakao kuwa watuhumiwa ni waganga wakuu wa wilaya na mikoa kwa kutoona na kutatua changamoto kabla hazijatokea.

Share: