Vietnam: rais wa urusi vladimir putin anatarajiwa kufanya mkutano na mwenyeji wake rais to lam

Rais wa Urusi Vladimir Putin yuko Vietnam, kituo chake cha pili cha ziara yake rasmi katika mataifa kadhaa ya Asia Mashariki.

Anatarajiwa kufanya mkutano na mwenyeji wake Rais To Lam na viongozi wengine wa chama cha kikomunisti Vietnam.

Marekani imekosoa ziara ya Bwana Putin Korea Kaskazini na katika mataifa mengine ya Asia kama jukwaa kwa kiongozi huyo wa Urusi kupata uungwaji mkono wa kuongeza makali katika vita dhidi ya Ukraine.

Vietnam bado inathamini uhusiano wa kihistoria ilionao nao na Urusi hata inajitahidi kuboresha uhusiano wake na Ulaya na Marekani.

Hapo jana Jumatano, Rais Putin na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un walitia saini makubaliano ya kulindana iwapo nchi zao zitakabiliwa na vitisho kutoka nje.

Uhusiano wa Vietnam na Urusi ni wa karibu na ulianza miongo mingi iliyopita, kwa misaada muhimu yaa kijeshi, kiuchumi na kidiplomasia iliyotolewa na Muungano wa Usovieti kwa jimbo jipya la kikomunisti huko Vietnam Kaskazini katika miaka ya 1950.

Share: