Uturuki imesimamisha uuzaji na uagizaji wa bidhaa zote zinazoingia na kutoka Israeli, kama hatua ya adhabu dhidi ya vita vya kikatili vya Tel Aviv dhidi ya Gaza ambavyo vimeua zaidi ya Wapalestina 34,596 katika kipindi cha miezi sita tu.
"Awamu ya pili ya hatua ya serikali imetekelezwa, na shughuli zote za usafirishaji na uagizaji bidhaa na Israeli zimesitishwa, zikijumuisha bidhaa zote," iliongeza.
Ankara mwezi uliopita iliweka vikwazo vya kibiashara kwa Israeli, ikieleza kuwa uamuzi huo utaendelea kuwepo hadi Israeli itakapotangaza kusitisha mapigano mara moja na kuruhusu uingizaji wa kutosha na usioingiliwa wa misaada ya kibinadamu Gaza.
Uturuki imekuwa mmoja wa wakosoaji wakubwa wa Israeli tangu ilipoanzisha kampeni ya kijeshi tarehe 7 Oktoba, huku ikitoa msaada mkubwa wa kibinadamu Gaza tangu kuanza kwa mashambulizi ya Israel, ikiwa ni pamoja na chakula, vifaa vya matibabu, na kuwahamisha maelfu ya wagonjwa.