Utawala wa kijeshi nchini burkina faso chini ya kapteni ibrahim traore, kusalia madarakani hadi 2029

Traore, ambaye pia ni mkuu wa nchi mwenye umri mdogo zaidi duniani, atakuwa uongozini kwa miaka mingine mitano baada ya kuafikiana kuongeza muda wa uongozi wa mpito wa taifa hilo kwa miezi 60, kuanzia Julai 2024.

Makubaliano hayo pia yanamruhusu Traore kuwania urais wakati uchaguzi utakapofanyika.

Kapteni Traore, maarufu kwa sare za kijeshi, alipanda ngazi na kuwa Kapteni mnamo 2020 kabla ya kuingia madarakani kwa kuogoza mapinduzi dhidi ya Luteni-kanali Paul Henri Sandaogo Damiba, Oktoba 2 2023.

Share: