
Emmanuel Macron na mkewe, Brigitte, wanapanga kuwasilisha ushahidi wa picha na kisayansi kwa mahakama ya Marekani kuthibitisha Bi Macron ni mwanamke.
Wakili wao anasema Rais wa Ufaransa na Bi Macron watawasilisha nyaraka hizo katika kesi ya kumharibia sifa dhidi ya mfuasi wa mrengo wa kulia Candace Owens baada ya kuendeleza imani yake kwamba Brigitte Macron alizaliwa mwanaume.
Mawakili wa Bi Owens wamejibu wakionyesha kuwa madai ya familia ya Macron ni ya uwongo.
Akizungumza na podikasti ya ‘BBC Fame Under Fire’, wakili wa familia ya Macron katika kesi hiyo, Tom Clare, alisema Bi Macron amechukulia madai hayo kuwa "ya kuhuzunisha sana" na yalikuwa "usumbufu" kwa rais wa Ufaransa.
Share: