Wakati huohuo maelfu ya watoto wengine wanaugua magonjwa ya kuambukiza na kuna ukosefu wa chakula, maji na dawa katika hospitali zilizofurika watu, chafu na hakuna makazi.
Shirika la juu la Umoja wa Mataifa linasema Ukanda wa Gaza ni sehemu hatari sana duniani ukiwa mtoto wakati mashambulizi ya kijeshi ya Israel katika eneo hilo yanaua na kujeruhi maelfu ya watoto.
Wakati huohuo maelfu ya watoto wengine wanaugua magonjwa ya kuambukiza na kuna ukosefu wa chakula, maji na dawa katika hospitali zilizofurika watu, chafu na hakuna makazi.
“Inaudhi sana kwamba wale wenye mamlaka wanapuuza wakati jambo hili baya linaathiri mamilioni ya watoto.” amesema James Elder, msemaji wa UNICEF, alipozungumza na wanahabari Jumanne mjini Geneva.
Elder hivi karibuni alirejea kutoka ziara ya wiki mbili huko Gaza.
Kwa mujibu wa wizara ya afya ya Gaza, inayo-ongozwa na Hamas, zaidi ya Wapalestina 19,400 wameuawa, ambapo takriban asilimia 70 ni wanawake na watoto, toka Israel ilipoanza mashambulizi yake ya mabomu na kulizingira eneo hilo ili kukabiliana na mashambulizi ya Oktoba 7 ya kundi la Hamas.