Unhcr ndani ya kilele cha mlima kilimanjaro

Kwa sasa Tanzania inahifadhi zaidi ya wakimbizi 240,000, wengi wao kutoka Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, huku zaidi ya nusu yao wakiwa ni watoto.

Wafanyakazi watatu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR nchini Tanzania wamepanda Mlima Kilimanjaro, ambao ni mlima mrefu zaidi barani Afrika, kwa lengo la kuchangisha fedha ili kusaidia uwekaji wa vifaa vya kuzuia radi katika shule zilizopo katika kambi za wakimbizi nchini Tanzania.

Safari yao ilichukua siku sita huku hatua ya mwisho ya kufikia mita 5,895 juu ya usawa wa Bahari ikianza usiku wa manane na kumalizika majira ya mapambazuko. Mvua kubwa na radi zimeleta madhara nchini Tanzania, hasa wakimbizi.

Damla Balaban, ambaye ameshiriki kupanda mlima ameeleza namna ambavyo timu ya UNHCR ilikumbushwa mara kwa mara juu ya hali halisi ya maisha katika kambi nyingi za wakimbizi pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo licha ya mandhari nzuri ya mlima Kilimanjaro jambo ambalo liliwapa motisha katika safari yao yote. 

Hakukuwa na chaguo la kuacha, kwa sababu lengo lilikuwa ni kuchangisha fedha kwa ajili ya usalama wa watoto wakimbizi” alisema 

Kwa sasa Tanzania inahifadhi zaidi ya wakimbizi 240,000, wengi wao kutoka Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, huku zaidi ya nusu yao wakiwa ni watoto. 

Share: