Uncrc imeonya juu ya hali ya kutisha, watoto milioni 24 wa sudan wapo hatarini

UNCRC imeripoti uwepo wa matukio mengi ya kikatili ikiwemo ubakaji wa Watoto, kuminywa kwa Haki za Binadamu

Wakati vita kati ya Jeshi la Sudan (SAF) dhidi ya Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) ikitarajiwa kuingia Mwaka wake wa pili Aprili 2024, Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Mtoto (UNCRC) imeonya juu ya hali ya kutisha kuhusu kizazi cha Taifa hilo kuelekea ukingoni. 

UNCRC imeripoti uwepo wa matukio mengi ya kikatili ikiwemo ubakaji wa Watoto, kuminywa kwa Haki za Binadamu, Watoto kukosa mahitaji ya Msingi na ukiukwaji wa Sheria za Kimataifa pamoja na ukiukwaji wa Haki za Watoto Kiuchumi na Kijamii

Ripoti hiyo imeeleza Watoto Milioni 24 wa Sudan wapo hatarini, kati yao Milioni 14 wakihitaji msaada wa haraka wa Kibinadamu na Milioni 4 wamekimbia makazi yao. 

Share: