Un yasema ukimwi unaweza kumalizwa ifikapo 2030

Ujumbe wa ripoti hii ni wa matumaini makubwa. Ingawa dunia kwa sasa haiko katika njia ya kukomesha UKIMWI kama tishio la afya ya umma.

Shirika la kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa, UNAIDS, lilisema katika Ripoti yake ya kila mwaka ya Siku ya UKIMWI Duniani kwamba majibu yanayoongozwa na jamii hayatambuliki, hayafadhiliwa ipasavyo na katika baadhi ya maeneo yanashambuliwa.

"Ujumbe wa ripoti hii ni wa matumaini makubwa. Ingawa dunia kwa sasa haiko katika njia ya kukomesha UKIMWI kama tishio la afya ya umma," ripoti hiyo ilisema.

Umoja wa Mataifa kwa mara ya kwanza uliweka lengo mwaka 2015 la kukomesha UKIMWI kama tishio la afya ya umma ifikapo 2030.

Kuna watu milioni 39 duniani kote wanaoishi na VVU - virusi vinavyosababisha UKIMWI. Kati yao, milioni 20.8 wako mashariki na kusini mwa Afrika na milioni 6.5 wako Asia na Pasifiki, Lakini kati ya milioni 39, milioni 9.2 hawana matibabu ya kuokoa maisha.

Share: