Ukienda shule unalipwa $25 kila wiki

Familia za kusini Carolina wanapata dollar 25 kwa wiki ikiwa watoto wao watajitokeza shule kila siku

Carolina Kusini imezindua mpango wa majaribio wa kupambana na utoro wa muda mrefu kwa kutoa zawadi za pesa taslimu kwa familia.

Wanafunzi wanaohudhuria shule kila siku katika wiki familia zao kupata au kulipwa $25 zaidi ya Tshs, 67,000 za Kitanzania kwa wiki hiyo.

Katika wiki yake ya kwanza, programu ililipa zaidi ya $30,000. — zaidi ya milioni 79 za Kitanzania, Takriban wanafunzi 1,900 katika shule kumi ni sehemu ya majaribio ya wiki tisa.

Pesa hizo hupakiwa kwenye kadi za benki na zinakusudiwa kusaidia kulipia gharama za kimsingi za maisha kama vile chakula, usafiri na huduma, wilaya inaripoti dalili za mapema za mafanikio, huku baadhi ya shule zikiona maboresho yanayoonekana katika mahudhurio.

Ikifadhiliwa na bajeti ya uendeshaji ya wilaya gharama ya jumla ya programu inatarajiwa kufikia takriban $400,000, sawa na zaidi ya bilioni 1 ya Kitanzania.

mpango huo unaendelea hadi katikati ya Mei ambapo wilaya itatathmini athari zake.

Share: