Misheni zote mbili za kidiplomasia mnamo Jumanne zilionya raia wao dhidi ya kuhudhuria mikusanyiko mikubwa, pamoja na shughuli za ibada.
Uganda imerekodi ongezeko la visa vya ukosefu wa usalama katika miezi ya hivi karibuni
Ubalozi wa Uingereza nchini Uganda umeonya kuhusu "tishio la ugaidi linaloongezeka nchini humo, ikiwa ni pamoja na kuwalenga wageni", saa chache baada ya ubalozi wa Marekani kutoa tahadhari kama hiyo.
Misheni zote mbili za kidiplomasia mnamo Jumanne zilionya raia wao dhidi ya kuhudhuria mikusanyiko mikubwa, pamoja na shughuli za ibada.
Pia walitahadharisha dhidi ya kushiriki katika tamasha za muziki na kitamaduni, kabla ya tamasha maarufu la Nyege Nyege mnamo Alhamisi.
Serikali ya Uingereza imewashauri raia wake dhidi ya kutembelea Mbuga ya Kitaifa ya Semuliki na Mbuga ya Kitaifa ya Queen Elizabeth, ambapo wanandoa wa Uingereza na Afrika Kusini na kiongozi wao wa Uganda waliuawa na kundi la wanamgambo wa Allied Democratic Forces (ADF) mwezi uliopita.
Kisha Uingereza ilionya raia wake dhidi ya kutembelea mbuga hiyo maarufu, Uganda imekumbwa na hali ya ukosefu wa usalama katika miezi ya hivi karibuni.
Mamlaka zilisema zilikomesha mashambulizi mawili tofauti dhidi ya makanisa yaliyofanywa na ADF mnamo Septemba na Oktoba, Mwezi Juni, wanamgambo wa ADF waliwaua watu 42 katika shule moja magharibi mwa Uganda, mojawapo ya mashambulizi mabaya zaidi ya ADF nchini humo.