Uganda imetajwa katika ripoti mpya ya umoja wa mataifa kwa kuwaunga mkono waasi wa m23

Nchi ya Uganda imetajwa katika ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 wanaofanya mashambulizi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Umoja wa Mataifa umesema kuwa Uganda imekuwa ikicheza katika mgogoro huo unaoikumba DRC katika majimbo ya Mashariki ambapo maelfu ya raia wameyakimbia makazi yao.

Kwa mujibu wa UN, Sultani Makenga Kiongozi wa M23 amekuwa akifanya safari zake nchini Uganda mara kadhaa hasa katika mji wa Entebbe na Kampala.

Kwa upande wa Uganda bado haijazungumza kitu chochote kuhusiana na ripoti hiyo mpya ya Umoja wa Mataifa.

Share: