Ufaransa itakuwa nchi ya 10 duniani kuwa na sheria ya kusaidia watu kufa

Rais Emmanuel Macron, ametangaza kuwa ifikapo Mei 2024, Serikali itawasilisha Bungeni Muswada wa Sheria itakayotoa Haki ya kusaidia Watu Kufa baada ya kuugua au kufikia hatua mbaya ya maumivu yasiyotibika

Macron amesema "Kutokana na kwamba kuna hali ambazo hauwezi kuzikabili kibinadamu, lengo letu ni kumpa Mtu uhuru binafsi wa kuamua kuhusu uhai wake baada ya kufikia hatua isiyo na nafuu au kupona"

Endapo Muswada huo utapitishwa, Ufaransa itakuwa nchi ya 10 duniani kuwa na Sheria ya Kusaidia watu Kufa. Nchi nyingine ni Uholanzi, Ubelgiji, Luxembourg, Colombia, Canada, Hispania, New Zealand, Ureno na Ecuador

Share: