Uchaguzi wa ubunge dr congo mahakama ya katiba yatangaza matokeo ya mwisho

Baadhi ya wabunge wapoteza viti vyao baada ya Mahakama ya Katiba kutangaza matokeo ya mwisho ya uchaguzi DR Congo.

Takriban wabunge 40 wapya watachukua nafasi za wenzao bungeni.

Mahakama ya Kikatiba ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo iliwabatilisha washindi wapatao arobaini kati ya 477 waliotangazwa washindi kwa muda na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi tarehe 13 Januari 2024.

Baada ya kusikiliza maombi yaliyowasilishwa mbele yake na miungano iliyokatishwa tamaa ambayo ilichagua kupinga matokeo ya muda ya uchaguzi wa hivi majuzi wa mwezi Disemba, Mahakama ya Katiba ya DRC pia ilithibitisha matokeo ya uhakika ya wabunge 477 watakaounda Bunge kwa miaka mitano ijayo.

Dieudonné Kamuleta, Rais wa Mahakama ya Katiba alisema walipokea jumla ya maombi 1,123 ya kupinga matokeo hayo, lakini ni maombi 43 pekee ndiyo yaliyoonekana kukubalika na kuasisiwa na Mahakama ya Katiba.

Uamuzi huo pia ndio ambao umekuwa ukisubiriwa na Rais Felix Tshisekedi, kabla ya kumteua Waziri Mkuu ambaye ataunda Serikali mpya.

Share: