Ubaguzi dhidi ya watu weusi waongezeka ulaya

Ni kulingana na uchunguzi wa wahamiaji Weusi wa kizazi cha kwanza na cha pili katika nchi 13 za Umoja wa Ulaya ambao umechapishwa leo Jumatano.

Hayo ni kulingana na uchunguzi wa wahamiaji Weusi wa kizazi cha kwanza na cha pili katika nchi 13 za Umoja wa Ulaya ambao umechapishwa leo Jumatano.

Shirika la Umoja wa Ulaya la Haki za Msingi (FRA) ambalo liliagiza uchunguzi huo na kuchambua ripoti ya matokeo yake, limesema katika muda wa miaka sita tangu uchunguzi wa awali, idadi ya waliohojiwa ambao walihisi kubaguliwa kwa msingi wa rangi yao katika miezi 12 iliyopita, iliongezeka kwa asilimia 10 na kufikia asilimia 34.

Nchini Ujerumani na Austria ubaguzi huo ulikadiriwa kuwa asilimia 64, hiyo ikiwa maradufu ikilinganishwa na asilimia 33 kwenye uchunguzi uliofanywa miaka sita iliyopita. Uchunguzi huo ulibaini kuwa ubaguzi huo umeongezeka pia Finland hadi asilimia 54.

Ripoti hiyo imetoa mapendekezo kwa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya ikiwemo kutekeleza ipasavyosheria dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Share: