Tumuombee rais samia akamilishe miradi ya maendeleo - mbunge cherehani

Watanzania wamehamasishwa kuendelea kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan ili aweze kutekeleza na kukamilisha miradi ya maendeleo anayotekeleza.

Rai hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Mhe. Dk. Emmanuel Cherehani alipoongoza harambee kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa Kanisa la Mtakatifu Theresia, Parokia ya Chona Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga.

Mhe. Cherehani amesema kuwa Mhe. Rais Dk. Samia amekuwa akitekeleza miradi mingi ya maendeleo nchini na katika Jimbo la Ushetu pia, huku akibainisha baadhi ya miradi hiyo ni kama ujenzi wa barabara, vituo vya afya, shule na madaraja ambapo miradi hiyo imelenga kuboresha maisha ya wananchi.

Share: