Tume ya umoja wa afrika (auc) yawataka waandamanaji nchini kenya kuwa watulivu

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC) Moussa Faki Mahamat amewataka washikadau kuwa watulivu na kukaribisha mazungumzo yenye tija ili kushughulikia masuala yenye utata yaliyosababisha maandamano nchini Kenya.

“Tunatoa wito kwa serikali na wananchi wa Kenya na kuwahimiza kudumisha amani, usalama na utulivu nchini,” alisema Faki katika taarifa.

Idadi ya watu waliouawa kwa kupigwa risasi wakati wa maandamano makubwa ya Jumanne haijathibitishwa huku baadhi yao wakiuguza majeraha ya risasi baada ya maafisa wa Kitengo cha Polisi cha Kupambana na Kutuliza Ghasia (ATPU) kuwafyatulia risasi.

Share: