Tume huru ya uchaguzi nchini rwanda imethibitisha wagombea wanane binafsi kuwania kiti cha urais julai 2024

Tume Huru ya Uchaguzi nchini Rwanda imethibitisha Wagombea wanane binafsi kuwania kiti cha Urais mwezi Julai 2024.

Hayo yametangazwa na Tume hiyo katika mkutano na waandishi wa habari wakati ikiweka wazi kuhusu maandalizi yalipofikia kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Tume hiyo Bi.Oda Gasinzigwa amesema kuwa kuna ambao walikiuka sheria ingawa hakuwaweka wazi.

Kampeni za Uchaguzi kwa upande wa Urais na Wabunge zitarajia kuanza nchini nzima Juni 22 hadi Julai 12 siku tatu kabla ya uchaguzi.

Share: