Travis scott afunguka kuwa na ndoto za kusomea uhandisi wa majengo

Mbali na muziki, msanii huyu anaonyesha mapenzi makubwa kwenye ujenzi na ana ndoto ya kuleta mabadiliko kwenye sekta hiyo siku za zijazo.

Msanii maarufu wa Hip-hop, #TravisScott, amefunguka kuhusu ndoto yake ya kusoma uhandisi wa majengo katika Chuo Kikuu cha #Harvard. Akiwa kwenye mahojiano na #Billboard, Travis alieleza jinsi alivyovutiwa na usanifu wa majengo anaposafiri duniani na kuona jinsi watu wanavyounda miundombinu kwa muda mfupi na kwa rasilimali chache.

Amesema kuwa, licha ya kuwa na uwezo wa kuchora michoro na kuunda mifano ya 3D, bado anahitaji kujifunza upande wa kiufundi ili kufanikisha mawazo yake kwa vitendo. "Ni mchakato mgumu sana," alisema Travis, akiongeza kuwa ana hamu kubwa ya kujua jinsi ya kupanga na kutekeleza miradi ya ujenzi.

Share: