Kuna imani kwa Toraja kwamba ukifa hutatengwa moja kwa moja na familia - unatarajiwa kuwaletea bahati nzuri na hivyo familia lazima ikuheshimu.
Kinyume na kanuni za Magharibi, watu wa Torajans, wanaoishi katika milima ya Sulawesi huko Indonesia, huwatendea jamaa zao wapendwa kana kwamba ni wagonjwa hawajafa. Katika Toraja, ni desturi ya kulisha marehemu kila siku na kuweka maiti kitandani katika chumba tofauti cha nyumba ya familia hadi familia iweze kumudu mazishi yanayofaa.
Kuna imani kwa Toraja kwamba ukifa hutatengwa moja kwa moja na familia - unatarajiwa kuwaletea bahati nzuri na hivyo familia lazima ikuheshimu.
Baada ya ibada ya mazishi ya "Rambu Solo", marehemu huzikwa makaburini. Lakini bado wanatembelewa kila mwaka mwezi agosti, kusafishwa na kupewa nguo mpya katika tambiko linalojulikana kama Ma’nene (‘Utunzaji wa Wahenga’).