
Muigizaji wa Marekani, Tom Cruise, ametunukiwa Distinguished Public Service Award, tuzo ya juu zaidi ya kiraia ya Jeshi la Wanamaji la Marekani, kwa mchango wake wa muhimu katika kuwakilisha wanajeshi kupitia uigizaji.
Tuzo hiyo ilitolewa na Waziri wa Jeshi la Wanamaji wa Marekani, Carlos Del Toro, katika shereheiliyofanyika London, ambapo Cruise anafanya kazi kwa sasa. Akiipokea tuzo hiyo, Cruise alisema kuwa anajivunia kutambuliwa huku akisisitiza heshima yake kwa wanajeshi.
Cruise, mwenye umri wa miaka 62, ameigiza kama Pete “Maverick” Mitchell kwenye filamu za 'Top Gun' ya 1986 na mwendelezo wake wa 2022. Filamu hizo zimeongeza uhamasishaji kuhusu Jeshi la Wanamaji, na kusababisha ongezeko la usajili wa wanajeshi.