Video hiyo ni maudhui ya kawaida yanayohusishwa na vita vya kisaikolojia dhidi ya Korea Kusini
Korea Kusini imesema itapiga marufuku wimbo wa propaganda wa Korea Kaskazini unaomsifu dikteta wa Pyongyang Kim Jong Un kama "baba rafiki" na "kiongozi mkuu".
Mdhibiti wa vyombo vya habari wa Seoul alisema video hiyo ya muziki, ambayo imekuwa maarufu kwenye TikTok tangu ilipotolewa Aprili, ni ukiukaji wa Sheria ya Usalama wa Kitaifa ya nchi hiyo.
"Wimbo huo unamsifu na kumtukuza Kim Jong Un," Tume ya Mawasiliano ya kuangazia Ubora ya Seoul ilisema katika taarifa siku ya Jumatatu.
Sheria ya Usalama inazuia ufikiaji wa tovuti na vyombo vya habari vya serikali ya Korea Kaskazini, na inaadhibu tabia na hotuba zinazopendelea utawala huo.
Toleo la 29 la video ya wimbo wa Baba Rafiki itazuiwa, tume ilisema, lakini haikufafanua jinsi hilo lingetekelezwa. Uamuzi huo ulichochewa na ombi kutoka Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi ya Korea Kusini, iliongeza.
"Video hiyo ni maudhui ya kawaida yanayohusishwa na vita vya kisaikolojia dhidi ya Korea Kusini, na ilichapishwa kwenye kituo kinachoendeshwa ili kufahamika kwenye ulimwengu wa nje na inalenga zaidi kumtukuza Kim," mdhibiti alisema.