Toeni taarifa mapema kwa vitendo viovu-dk.mwinyi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi amewataka wananchi kutoa taarifa mapema kwa vitendo ambavyo vinafanyika kinyume na maadili pamoja na hali ya usalama katika jamii. 


Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo wakatu alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika sala ya Ijumaa msikiti wa Mushawar Mwembeshauri tarehe 21 Juni 2024.

Aidha Rais Dkt.Mwinyi amewapongeza wananchi kwa kuendelea kudumisha amani na utulivu nchini.

Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa Serikali imejipanga kwa kufanya operesheni maaluum ya kuimarisha hali ya ulinzi na usalama nchini kupitia kamati za ulinzi na usalama za Mikoa na Wilaya. 


Rais Dkt.Mwinyi amewahimiza waumini wa dini ya Kiislamu kuendelea kutenda mambo mema na kujiepusha na maovu.

Share: