Tiktok yarejesha huduma zake Marekani kwa msaada wa Donald Trump

Masaa machache tu baada ya kusitisha huduma kufuatia marufuku nchini Marekani, Mtandao wa TikTok umetangaza kuwa inarejesha huduma kwa watumiaji wake wa Marekani huku ikimshukuru Rais mteule Donald Trump kwa msaada wake.

Jioni ya Jumamosi (Januari 18), kampuni ya ByteDance yenye makao yake nchini China ilianza kuondoa upatikanaji wa programu zao za TikTok, CapCut, na Lemon8 nchini Marekani. Asubuhi ya Jumapili (Januari 19), kampuni hiyo ilianza kurejesha huduma kwa watumiaji wake wa Marekani na kutoa taarifa rasmi.

Katika ujumbe uliochapishwa na #TikTokPolicy kwenye X, ulisema ,

“Kwa makubaliano na watoa huduma wetu, TikTok iko katika mchakato wa kurejesha huduma. Tunamshukuru Rais Trump kwa kutoa ufafanuzi na uhakikisho muhimu kwa watoa huduma wetu kwamba hawatakumbwa na adhabu yoyote kwa kutoa TikTok kwa Wamarekani zaidi ya milioni 170 na kuruhusu zaidi ya biashara ndogo ndogo milioni 7 kustawi.”

Share: