Tekashi 69 akiri makosa apunguziwa kifungo

Rapper kutoka NewYork City Marekani Daniel Hernandez maarufu kama Tekashi @6ix9ine ametajwa kukiri makosa yake (plea deal) nakutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi jambo litakalo mpunguzia adhabu ya kukaa jela kwa muda mrefu na badala yake atakaa kwa siku 30 tu, na kutumikia kifungo cha nje.

Wakili wa Marekani alipendekeza kufungwa mara moja, na mwaka wa ziada wa kuachiliwa kwa kusimamiwa ufuate. Baada ya kuachiliwa, atakabiliwa na siku 90 za vizuizi zaidi: siku 30 za kwanza chini ya kifungo cha nyumbani, 30 zinazofuata chini ya kizuizi cha nyumbani, na 30 za mwisho na amri ya kutotoka nje. Kupitia "tmz_tv"


69 alikamatwa mapema mwezi uliopita kwa kukiuka masharti ya kifongo chake cha nje ,ambacho alipewa baada ya kukiri makosa ya kuongoza genge la wahuni la Nine Trey Gangsta Bloods (NTG) 2019 na kuepuka kifungo cha mika 47 mpaka kifungo cha maisha jela.

Share: