
Taylor Swift ametangazwa kuwa mbabe wa Billboard Music Awards (BBMAs) 2024, Desemba 12. Taylor Swift ameibuka na ushindi wa tuzo 10 mpya, na kufikisha jumla ya ushindi wa tuzo 49, idadi kubwa zaidi kuwahi kufikiwa na msanii yeyote kwenye historia ya BBMAs.
Miongoni mwa tuzo zake ni Msanii Bora ambayo ameshinda kwa mara ya nne, rekodi ya kipekee, Msanii Bora wa Kike, na Msanii Bora wa Billboard 200.
Kabla ya ushindi huu, Taylor Swift alikuwa amefungana na Drake, kila mmoja akiwa na tuzo 39. Mwaka huu, Drake ameshinda tuzo tatu, na kufikisha jumla ya tuzo 42.
Share: