TANZANIA YA PATA SIFA KABAMBE KUWA NI NCHI AMBAYO NI KIELELEZO CHA AMANI

Bw. Kombos, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Cyprus, yuko nchini Tanzania kwa ziara ya siku tatu.

Mwakilishi Rasmi wa Makamu wa Rais wa Tume ya Ulaya na Mwakilishi Mkuu wa Masuala ya Kigeni na Sera za Usalama, alieleza kuthamini kwa EU mafanikio ya Tanzania katika kudumisha amani na utulivu wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.


Umoja wa Ulaya (EU) umeisifu Tanzania kwa kudumisha hadhi yake kama kielelezo cha amani katika eneo la Afrika Mashariki, huku ukiitakia nchi hiyo mchakato wa uchaguzi mkuu ujao uwe wa haki na wa amani, ili kuimarisha demokrasia na ukuaji wa uchumi.


“Tunaiona Tanzania kama mshirika muhimu wa kimkakati, nchi tulivu na yenye amani, ikiwa na ukuaji mkubwa wa uchumi na idadi ya watu katika ukanda huu unaokabiliwa na changamoto nyingi,” alisema.

Hivyo basi, alitoa hakikisho kuwa Tanzania itaendelea kufaidika na ushirikiano wa kimkakati kwa maendeleo ya pande zote kati ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki na Umoja wa Ulaya.


Akifafanua kuhusu ushirikiano wa pande mbili unaoendelea, alieleza kuwa Tanzania imenufaika na mpango wa EU wa Global Gateway, hususan katika uendelezaji wa miundombinu ya kiuchumi na rasilimali muhimu, huku ikijitokeza kama mnufaika mkubwa wa mpango huo.

Share: