Tanzania itaendelea kumuenzi shujaa wa taifa hili edward moringe sokoine

Edward Moringe Sokoine alikuwa mwanasiasa aliyepambana na rushwa, wizi na unyonyaji hakutaka mzaha hata kidogo.

Alihudumu kwa vipindi viwili kama Waziri Mkuu wa Tanzania, kuanzia Februari 13, 1977, hadi Novemba 7,1980, na Februari 24, 1983, hadi Aprili 12, 1984.

Alijulikana kwa bidii katika kazi yake na hotuba zake za Hamasa zilizogusa nyoyo za wananchi.

Aprili 12, 1984 ilikuwa siku ya simanzi kwa Watanzania ambapo Edward Moringe Sokoine alifariki Dunia kwa ajali mbaya ya gari akiwa njiani akitokea Dodoma kuelekea Dar es Salaam akiwa na umri wa miaka 45 tu na kuacha Wake wawili na watoto kumi na moja.

Tanzania inaendelea kumuenzi Edward Sokoine kwani alikuwa kiongozi aliyekuwa na bidii katika kazi yake, mwadilifu, muwazi, mzalendo kwa nchi yake, na alionesha uhalisia wake katika hotuba zake mbalimbali alipokuwa akizungumza na wananchi na viongozi katika matukio mbalimbali.

Share: