Tanzania imepokea tsh. bilioni 8.9 kwaajili ya mradi wa ukarabati wa bandari ya kigoma

Tanzania imepokea msaada wa nyongeza wa Yen za Japan Milioni 548 (Tsh. Bilioni 8.9) kwa ajili ya mradi wa ukarabati wa Bandari ya Kigoma baada ya marekebisho ya mikataba miwili ya msaada kati ya Tanzania, Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) na Ubalozi wa Japan. 

Mikataba hiyo imesainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, Balozi wa Japan nchini Tanzania, Yasushi Misawa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan Tanzania, Hitoshi Ara kwa niaba ya Japan. 

Dkt. Mwamba amesema, awali Serikali ya Japan kupitia mikataba iliyosainiwa Februari 4, 2022 ilitoa msaada wa Yen za Japan Bilioni 2.73 (Tsh. Bilioni 44.42) kwa ajili ya ukarabati wa Bandari hiyo, hivyo jumla ya msaada waliotoa ni Tsh. Bilioni 53.35.

Share: