Tamisemi: watendaji wa vijiji 1,986 kupata ajira

“Katika mwaka 2023/24 maafisa tarafa 63 kati ya nafasi wazi 84 wameajiriwa na kupangiwa vituo vya kazi. Aidha, katika kuboresha utendaji kazi, umefanyika msawazo wa watumishi wa halmashauri zilizokuwa na watumishi wengi na kuwahamishia halmashauri zenye upungufu wa watumishi ambapo watumishi 646 walihamishwa. Vilevile, Ofisi ya Rais – TAMISEMI inakamilisha taratibu za kuajiri watendaji wa kata 525, watendaji wa vijiji 1,986, watendaji wa mitaa 1,333 na maafisa tarafa 21” 

Amesema Mohammed Mchengerwa, Waziri wa Nchi, OR - TAMISEMI wakati akisoma hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa mwaka wa Fedha 2024/2025 Bungeni jijini Dodoma.

Share: