Taasisi ya chakula na lishe kibaha yafutwa

Msajili wa Hazina ameshaelekezwa kukamilisha taratibu husika za makabidhiano na Wizara ya Afya, Mkumbo amewaambia Wanahabari jijini Dar es Salaam.

Shirika la Elimu Kibaha (KEC) sasa litavunjwa na kuwa Shule ya Sekondari na Chuo cha Ufundi kwa muujibu wa maamuzi yaliyotangazwa na serikali Ijumaa Disemba 15.

Waziri wa Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo amesema kutokana na uamuzi huo Hospitali ya Tumbi - Kibaha haitakuwa sehemu ya Shirika hilo bali hospitali ya Mkoa wa Pwani.

“Msajili wa Hazina ameshaelekezwa kukamilisha taratibu husika za makabidhiano na Wizara ya Afya,” Mkumbo amewaambia Wanahabari jijini Dar es Salaam.

Pia amesema Serikali imefuta Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC). Kwa mujibu wa Mkumbo, maamuzi hayo ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais Samia Suluhu Hassan la kutaka kufanyika mageuzi makubwa katika uendeshaji wa mashirika na taasisi za umma.

Share: