Sweden yavuka kihunzi kingine uanachama wa jumuiya ya nato

Uturuki, moja ya mataifa 31 wanachama wa NATO, imechelewesha kwa karibu mwaka mmoja maombi ya kujiunga kwa Sweden baada ya kuituhumu nchi hiyo kutochukua hatua stahiki dhidi ya makundi yanayotishia usalama wa Uturuki.

Kamati ya Mambo ya Kigeni ya Bunge la Uturuki imeridhia maombi ya Sweden kujiunga na Jumuiya ya Kujihami ya NATO, uamuzi unaoongeza matumaini kwa taifa hilo kukaribia kuwa mwanachama kamili wa mfangamano huo wa kijeshi.

Itifaki ya maombi ya uanachama wa Sweden sasa itasubiri kuidhinishwa na bunge zima la Uturuki ikiwa ni hatua ya mwisho kwa mchakato huo. Bado hakuna tarehe rasmi iliyopangwa kwa ajili ya kura hiyo.

Uturuki, moja ya mataifa 31 wanachama wa NATO, imechelewesha kwa karibu mwaka mmoja maombi ya kujiunga kwa Sweden baada ya kuituhumu nchi hiyo kutochukua hatua stahiki dhidi ya makundi yanayotishia usalama wa Uturuki.

Miongoni mwa makundi hayo ni ya wanamgambo wa Kikurdi na mtandao wa wafuasi wengine wa upinzani unaoshukuwa kuwa sehemu ya jaribio la mapinduzi la mnamo mwaka 2016 nchini Uturuki.

Share: