Sunak: uingereza itasimama kidete na ukraine

Taarifa ya ofisi ya waziri mkuu huyo imesema Sunak ametoa ahadi ya msaada wa kijeshi na uungaji mkono wa kidiplomasia.

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak aonesha dhamira ya dhati ya taifa lake kuisaidia Ukraine katika mapambano yake dhidi ya Urusi.Kauli hiyo ameitoa wakati wa mazungumzo ya simu na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.

Taarifa ya ofisi ya waziri mkuu huyo imesema Sunak ametoa ahadi ya msaada wa kijeshi na uungaji mkono wa kidiplomasia. Wakati wa mazungumzo yao ya simu, Sunak alitoa salamu za rambirambi kwa raia wote wa Ukraine waliouawa na kujeruhiwa katika mashambulizi ya kinyama ya anga ya Urusi katika kipindi cha Krismasi. Wiki iliyopita serikali ya Uingereza ilitangaza kuwa itatuma takriban makombora 200 ya ulinzi wa anga nchini Ukraine kutokana na hali ya mashambulizi ya hivi karibuni ya Urusi.

Share: