Somalia yajiunga uanachama wa afrika mashariki (eac)

Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika Jijini Arusha nchini Tanzania, umeridhia Nchi ya Somalia kujiunga na EAC na sasa inakuwa Mwanachama wa nane wa Jumuiya hiyo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki January Makamba ni miongoni mwa Viongozi waliotoa pongezi za awali kabisa kwa Somalia kuridhiwa kuwa Mwanachama mpya wa EAC ambapo ameitakia kheri Somalia katika kuielewa na kuiishi pamoja na kuitekeleza misingi ya EAC na itifaki zake katika kukuza na kuendeleza Jumuiya hiyo.

Katika hatua nyingine mkutano huo pia umemtangaza Rais wa Sudan, Salva Kiir Mayardit kuwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Itakumbukwa katika mkutano kama huo mwaka jana aliyekuwa Rais wa Kenya na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo wakati huo, Uhuru Kenyatta alitangaza rasmi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kujiunga na EAC.

Share: