Somalia imekuwa mwanachama kamili wa jumuiya ya afrika mashariki

Somalia imekuwa mwanachama kamili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) baada ya kukamilisha hatua zote zinazohitajika ili kuidhinishwa kuwa mwanachama kwa jumuiya hiyo ya kikanda.

Usimamizi wa EAC Jumatatu ilichapisha kwenye matandao wa X, zamani Twitter, kwamba Somalia imepata uanachama kamili "baada ya kuwasilisha Hati yake ya Kuidhinishwa kwa Katibu Mkuu" wa jumuiya hiyo.

Chombo cha uidhinishaji ni hati rasmi iliyotolewa na nchi, ambayo inakubali kufungwa na mkataba.

Novemba mwaka jana, wakuu wa nchi nyingine wanachama wa EAC walikubali kujumuishwa kwa Somalia katika umoja huo.

Somalia inakuwa mwanachama wa nane wa EAC baada ya Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kenya, Sudan Kusini, Tanzania, Rwanda na Uganda.

Hatua hiyo inanuiwa kuimarisha ukuaji wa uchumi nchini humo, ambao bado unaendelea kuimarika kutokana na miongo mitatu ya vita.

Share: