SOMA : HUKUMU YA DIDDY IMEWADIA

Kikao kilichopangwa Jumanne alasiri kusikiliza hoja za Sean “Diddy” Combs kuhusu ombi la kupewa tarehe ya hukumu mapema kilisitishwa bila hoja yoyote kuwasilishwa wala tarehe mpya kuwekwa.

Wakili wa utetezi na waendesha mashtaka wa serikali walikubaliana awali tarehe ya hukumu iwe Septemba 22 kwa mujibu wa barua ya pamoja iliyowasilishwa Jumanne kabla ya kikao cha simu. Hata hivyo, muda mfupi kabla ya kikao, mawakili wa pande zote walituma barua nyingine ya pamoja kwa Jaji Arun Subramanian wakisema wamekubaliana tarehe awali ya jaji ya Oktoba 3.


Wakili wa utetezi Marc Agnifilo na mwanasheria wa mashtaka Christy Slavik walihudhuria kikao hicho cha simu wakati msaidizi wa mahakama alikata kikao ili kuuliza kama kuna jambo lolote zaidi la kujadili zaidi ya tarehe ya hukumu. Walipojibu kuwa hakuna, msaidizi huyo alisitisha kikao na kuwaarifu kuwa Jaji Subramanian atawajibu kwa maandishi.

Kwa sasa, Jaji Subramanian ameweka tarehe ya hukumu ya Sean Combs kuwa Oktoba 3, kama ilivyoelezwa kwenye rekodi za mahakama.


Tufatilie kupitia kisumbuzi @startimestz CH 161 (antena) CH 401 (Dish) pamoja na kwenye YouTube channel yetu ya #STBongoTV Kwa Taarifa zaidi.

#STBongoUpdates #NyumbaniKwanza

Share: